Science-backed methods
Mbinu zenye msingi wa kisayansi - Elewa dhana za emalsheni, uhifadhi na kiwango cha pH ili bidhaa zako ziwe salama, imara na tayari kuuzwa.
Kundi jipya la mafunzo ya vipodozi vya nywele kwa nadharia linaanza hivi karibuni — jiandikishe sasa uanze kujifunza.
Tunakuwezesha kujifunza mbinu na sayansi za utengenezaji wa vipodozi vya asili kwa ngozi na nywele, ili uweze kutengeneza bidhaa salama na kuanzisha biashara yenye mafanikio.
wanafunzi 2,400+ wanatengeneza vipodozi vya asili kwa kujiamini
Kozi
Formula zipo tayari
Wanafunzi waliopo sasa
Wameridhika na kufurahia
AsiliSpot Formulation Organization ni kituo cha mafunzo kinachowawezesha wajasiriamali kujifunza sayansi na mbinu za kutengeneza vipodozi vya asili salama kwa ngozi na nywele. Tangu kuanzishwa mwaka 2020, tumekuwa tukitoa maarifa ya vitendo yanayowaandaa wanafunzi kuunda bidhaa bora na kuanzisha biashara zao.
Kupitia mafunzo yetu ya mtandaoni na ana kwa ana, tumefikia zaidi ya wanafunzi 2,000, tukijenga kizazi cha watengenezaji wa vipodozi wenye ujuzi, wakisaidiwa na fomula, ushauri na malighafi bora kwa ajili ya ukuaji wa biashara zao.
Kuunda vipodozi vya asili kwa elimu, ubunifu na ujuzi wa vitendo wa hali ya juu.
Fomula safi, maarifa sahihi na athari chanya kwa jamii.
Tunachanganya sayansi ya vipodozi, mafunzo ya vitendo na jamii inayotoa sapoti, ili usihisi kukwama.
Mbinu zenye msingi wa kisayansi - Elewa dhana za emalsheni, uhifadhi na kiwango cha pH ili bidhaa zako ziwe salama, imara na tayari kuuzwa.
Fuata formula sahihi, zenye hatua halisi unazoweza kuzitumia kutengeneza vipodozi vya asili peke yako.
Pata mrejesho kuhusu fomula zako na ubadilishane mawazo na wabunifu wenzako walio kwenye jumuiya yetu.
Pata access ya masomo ya nadharia na vitendo kwa kipindi chote cha mafunzo online, jifunze kwa kasi yako mwenyewe.
Pata viambato vinavyozingatia maadili na uhifadhi wa mazingira, na upunguze taka kupitia mbinu nzuri katika utengenezaji wa bidhaa.
Masomo ya ziada kuhusu packaging, ukokotoaji wa gharama na uuzaji — geuza shauku yako kuwa biashara halisi.
Kozi madhubuti zitakazokuongoza kutoka hatua ya uzalishaji wa awali kabisa hadi kwenye bidhaa tayari kwa mauzo. Bofya kozi yoyote ili kuona mtaala wake kamili.
Mchanganyiko wa fomula za hali ya juu na zilizolengwa mahususi kwa ajili ya watengenezaji ambao tayari wanaelewa misingi ya formulation na wanataka miongozo madhubuti ya kuanzia kwa ajili ya kutengeneza bidhaa maalum za asili za vipodozi.
Join the ASILISPOT Professional Formulators Community for expert guidance when your formula separates, your pH shifts, an ingredient needs replacing, or you want confidence before manufacturing.
Njia kamili ya masomo, kuanzia mwanzo mpaka kutengeneza bidhaa yako ya kwanza
Jiunge na ndani ya mda mfupi utaweza kuandikishwa kwenye darasa
Masomo ya video na machapisho, kukufundisha mambo ya msingi katika uundaji wa bidhaa
Fuata hatua kwa hatua formula zilizoandaliwa na utengeneze bidhaa yako ya kwanza
Pata mrejesho kutoka kwa mkufunzi, jipatie cheti chako, na ujifunze jinsi ya kuuza unachotengeneza
Habari, mimi ni Mecktilda — mtaalamu wa kemia ya vipodozi na mwanzilishi wa chapa ya bidhaa za asili za kutunza ngozi. Nimetengeneza fomula nyingi za bidhaa na kutoa mafunzo kwa watengenezaji mbalimbali nchini kote. AsiliSpot, hurahisisha dhana tata za kemia na kuzigeuza kuwa hatua rahisi zinazoweza kufuatwa kwa urahisi, ili uweze kutengeneza bidhaa kwa kujiamini.
“Sikuwa na bidhaa zinazofaa, baada ya kujifunza AsiliSpot, hatimaye nikawa na mkusanyiko kamili wa bidhaa za utunzaji wa ngozi ambazo sasa ninaziuza masokoni. Formula ya utengenezaji na maoni ninayopokea ni ya thamani kubwa sana.”
“Hatimaye, dhana ya kemia imeeleweka. Mecktilda anaelezea kuhusu uhifadhi na kiwango cha pH kwa namna ambayo nimeielewa kweli..”
"Nimejifunza na nina uwezo wa kutazama tena notes zangu na kuweza kurejea masomo wakati wowote ninapofanya utengenezaji wa bidhaa.”
Hapana kabisa. Programu yetu ya wanaoanza haihitaji ujuzi wowote wa awali na inakuongoza hatua kwa hatua kuanzia vifaa hadi kukamilisha bidhaa yako ya kwanza.
Unaweza kuanza na vifaa vya msingi ambavyo vitaainishwa mwanzoni mwa kozi. Ni vya kawaida kama vile vya jikoni, na vya ziada vitakavyoorodheshwa.
Ndiyo. Tunafundisha mbinu bora za kuhifadhi bidhaa na kuhakikisha uthabiti na usalama, pamoja na sehemu ya ziada kuhusu kuzingatia kanuni na uwekaji lebo ili uweze kuuza bidhaa zako vyema.
Unaweza kutazama materials ya kozi kama vile machapisho na video katika kipindi cha kozi kilichowekwa. Unashauriwa kuandika notes ili kutunza kumbukumbu ya formula zote na ujuzi utakaojifunza
Ndiyo - Utakapokamilisha kozi yoyote utapewa cheti kutoka AsiliSpot Formulation Organization kuthibitisha maarifa na ujuzi wako mpya
Wasiliana na timu yetu ya kusaidia wanafunzi, nasi tutakusaidia kuchagua kozi inayofaa na kuanza.
Arusha, Tanzania
Mon – Sat, 8:00 – 18:00 EAT
Jiunge na maelfu ya watengenezaji wanaojifunza kutengeneza bidhaa safi na madhubuti za utunzaji wa ngozi na nywele — huku wakitengeneza kwa kujiamini.
Ni wewe tuuu.